imetumwa na mtumishijasiri 23 Mei 2015
Mshirikishe mwenzako
Watu wanaohama mji wa Ramadi
Mratibu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini iraq amesema
kuwa huenda takriban watu 40,000 wameukimbia mji wa Ramadi ambao
ulitekwa na wanamgambo wa islamic state karibu wiki moja iliyopita.
Dominik
Bartsch aliiambia BBC kuwa watu wengi waliokimbia makwao wakiwemo
watoto, watu wazee na wagonjwa wamekwama kwenye daraja moja linaloingia
mjini Baghdad bbada ya kuzuiwa kuingia mji huo.
Anasema kuwa kuna ripoti kwamba baadhi ya watoto wameaga dunia baada ya kuishiwa na maji mwilini.
Bwana
Bartsch pia anasema kuwa umoja wa mataifa una wasi wasi kuhusu hatma ya
wakimbizi waliojikuta kati kati ya mapigano kati ya wanamgambo wa
Islamic State na vikosi vya serikali.
www.mtumishijasiri.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.