Islamic State yasajili watoto wadogo kufanya ugaidi
kwa picha hizo bonyeza HAPA--->http://mtumishijasiri.blogspot.com/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/06/02/150602044752_syria_child_soldiers_512x288_mtumishijasiri_nocredit.jpgUmoja wa Mataifa umeishutumu IS na makundi mengine yenye silaha nchini Syria na Iraq kwa kuwatesa na kuwaua watoto.
Watoto walisajiliwa, kufunzwa na kutumiwa katika uwanja wa vita.
Kijana mwingine ameiambia BBC namna alivyopigana na kuua kwa ajili ya kikundi cha al-Nusra Front chenye uhusiano na al-Qaeda. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 tu na wakati huo alipojiunga na IS alimkuta kijana wa miaka 13 akifundishwa itikadi kali ya kidini.
Amefungwa kitambaa usoni, na wanaume wawili wakiwa wameficha sura zao, wakiwa wamevaa nguo nyeusi kutoka juu hadi chini ya vidole vya miguu. Mmoja ana kifu na bastola na mwingine ana hangaika chumbani akiwana bunduki aina ya AK-47.
Ndani ya maeneo waliyojitangzia kuyatawala, Islamic State imeondoa mfumo wa elimu ya kawaida na badala yake kuanzisha shule za mtindo wa kijeshi ambazo zinawafundisha watoto iutikadi kali ya kidini
na kuwafundisha kuua.
Islamic State wamekuwa wakiua nchini Syria na Iaraq, lakini madhara yake yataonekana zaidi baadaye.
Huu ni ufisadi wa karne. Watoto wa IS watakua kuwa watu wazima wakiwa wamefundishwa kuua na kujaa chuki na watazisumbua Syria na Iraq kwa miaka mingi ijayo.
mtumishijasiri.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.