Tuzo 6 za Alli Kiba zasababisha Kauli Hizi Toka kwa Wema na Jokate
Jokate ambaye anatajwa kuwepo mapenzini na Ali Kiba sasa hivi aliandika >>> ‘Hongera Sana Cherie @officialalikiba Kwa Kujishindia Tuzo Sita Jana Usiku Kwenye Kiba Tanzania Music Awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2015. Teh teh teh. Ni Kitu Cha Kumshukuru Mungu Ulikaa Kimya Miaka 3 Ila Ukarudi Na Wimbo Mmoja Ukatuteka Tena’
‘Kusema Ukweli Tukiachilia Mbali Ushabiki ‘Mwana’ Ulituliza Akili Na Ukafanya Vizuri Sana Nchini. Mashabiki Wanakupenda. Sana. Mpole Hivi, Mcheshi, Mstaarabu. Na Unajua Mziki. Tunakuombea Sasa Hii Iwe Motisha Ya Wewe Kufika Mbali Zaidi. Ndio Kwanza Safari Imeanza. Uzuri Unaomba Mungu So Najua Hata Kutupa. Ila Kaza Mwana We Kazaaa!!! tuko nyuma yako
’ – Jokate
Wema Sepetu aliandika >>> ‘Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha’
Baada ya Jokate kupost picha ya Kiba na hayo maneno hapo juu…… post iliyofata aliweka picha yake yeye na Wema na kuandika >>> ‘Ni kitu kizuri na chenye nguvu pale Wanawake hodari wanaoungana‘
Ali Kiba mwenyewe baada ya ushindi huu aliandika “Ningependa Kuchukua Nafasi Hii Kutoa Shukrani Zangu Kwanza, Kwa MUNGU Muumba Aliyenipa Kipaji Hiki, Pili Familia Yangu Kwa Kuniongoza Na Kunipa Moyo Wa Kufanya Kazi Zaidi, My Management, Asante Kwa Kuniongoza Vyema. Mashabiki Zangu Wa Dhati Asanteni Sana Kwa Kuthamini Kipaji Changu Na Kupenda Kazi Zangu! Nawapenda Na Kuwashukuru From The Bottom Of My Heart. MUNGU Awabariki Sana …#KingKiba
0 comments:
Post a Comment