HATIMAYE RAIS KIKWETE AMTANGAZA MRITHI WAKE RASMI
MWANANCHI
Hatimaye Rais Jakaya Kikwete
amemtaja mrithi wake baada ya kuwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM kumchagua mgombea urais anayekubalika ndani na nje ya chama hicho.
Kikwete alisema hayo jana wakati
akifungua kikao cha Halmashauri Kuu kwenye ukumbi wa ofisi ya makao
makuu ya chama hicho mjini hapa, unaojulikana kwa jina la White House.
Kauli hiyo imekuja wakati chama hicho
kikiwa kwenye wakati mgumu kupata mgombea mpya baada ya Rais Kikwete
kumaliza muda wake wa vipindi viwili vinavyokubalika kikatiba, huku
kukiwa na ongezeko kubwa la nguvu ya upinzani.
Juzi, Kamati Kuu ya CCM iliwaachia huru
makada wake sita waliotumikia adhabu ya miezi 17 ya kuzuiwa
kujishughulisha na shughuli za uchaguzi baada ya kubainika kukiuka
sheria za uchaguzi za chama hicho kutokana na kuanza kampeni mapema.
Miongoni mwa makada hao, wamo wanaopewa
nafasi kubwa ya kupitishwa na chama hicho na ambao kambi zao zimekuwa
zikipambana vikali na kuweka wasiwasi wa kuivuruga CCM.
Lakini Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa
chama hicho, alionekana kufahamu hali inayoendelea na alitumia muda huo
kueleza jinsi ambavyo CCM imejidhatiti kupata mgombea urais kwa
kuzingatia maslahi ya chama hicho na ya Watanzania, akisema wakati wa
kudhani mtu yeyote anayeteuliwa na chama hicho atachaguliwa na wananchi
umeshapita.
Rais Kikwete alisema kikao cha
Halmashauri Kuu kina umuhimu wake kwa sababu kitaamua ushiriki wa CCM
katika Uchaguzi Mkuu na kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea wa chama
hicho.
Rais Kikwete alisema watu wote wanachama na wasio wanacham wanasubiri kwa hamu uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.
“Watanzania
wote bila kujali itikadi zao wanaitazamia na kuitumainia CCM kutoa
uongozi ulio bora kwa nchi yetu. Hali hii inathibitisha uleusemi wa Baba
wa Taifa kwamba Rais anaweza kutoka chama chochotelakini rais bora
atatoka CCM,”.
Alisema CCM inatakiwa kutambua na
kuzingatia uzito wa wosia huo wBaba wa Taifa na kuhakikisha kuwa
unatekelezwa kwa ukamilifu wake.
“Asiyesikia
la mkuu huvunjika guu. Vikao vya Kamati Kuu, HalmashauriKuu ya Taifa na
Mkutano Mkuu wa Taifa, vina jukumu maalumu la kuongozna kusimamia
mchakato wa uteuzi ndani ya chama, utakaotuwezeshkupata wagombea
wanaofaa,”alisema.
“Wenye
kukidhi kiu na matarajio ya wanachama wa CCM na wananchi waJamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ni sisi. Lazima tupate wagombewanaochagulika,
tunapowapeleka kwa wananchi ambao wengi wao siywanaCCM.”
www.mtumishijasiri.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.