Huu ndio mkanganyiko ulioko ndani ya baraza la senate uko Marekani juu ya sheria ya ugaidi
01 june 2015..mtumishijasiri
Baraza la Senate la Marekani
limeshindwa kuzuia kumalizika kwa muda wa saa mbili wa sheria ya
kupambana na ugaidi ambapo Shirika la Usalama wa Taifa linakusanya kwa
wingi taarifa katika simu za raia wa Marekani.
Katika mjadala wa Jumapili ambao ni nadra wajumbe wa Senate hawakukubali kuongezea muda wa kuendelea kwa sheria ya sasa ikiwepo migawanyiko miongoni mwa wajumbe wa chama cha Republican kwa kushindwa kuafikiana.
Baraza la Senate kwa sasa linajadili Muswada wa kuanzisha ufuatiliaji wa hatua za karibu zaidi.
Muswada ambao umekwisha pitishwa na Baraza la Wawakilishi.
Rais Obama na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani,CIA, John Brennan, wameonya kuwa kushindwa kupitisha upya kwa hatua za ufuatiliaji vitendo vya kigaidi kutaifanya nchi kushindwa kufuatilia vitisho vya kigaidi.
mtumishijasiri.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment